MKUTANO MKUU Maalum XVI wa KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria umemchagua Mchungaji OSCAR ITAEL LEMA kuwa Askofu wa Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria. Zoezi la uchaguzi limeongozwa na Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Daktari ALEX GEHAZ MALASUSA. Jumla ya wajumbe 223 wamepiga kura. Askofu mteule amechaguliwa kwa kura 121 na Msaidizi wa Askofu Mteule amechaguliwa kwa kura 165. Aidha, Askofu Daktari Alex Malasusa amehimiza mshikamano, umoja ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa mujibu wa katiba ya Kanisa. Askofu Mteule Oscar Itael Lema ameahidi ushirikiano katika kutokomeza ukabila ndani ya Kanisa. Kaimu Katibu Mkuu wa Dayosisi Ndugu. Joshua Kyelekule ameeleza kuwa, zoezi zima la uchaguzi limefanyika kwa kuzingatia Katiba ya Dayosisi. Mchanganuo wa Matokeo ya Uchaguzi ni kama ifuatavyo: Jumla ya Wapiga kura =223. 1:Mchungaji Oscar Lema Kura = 121 2.Mchungaji Stephano Ling'hwa kura = 102 .