MKUTANO MKUU Maalum XVI wa KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria umemchagua Mchungaji STEPHANO LING'HWA kuwa Msaidizi wa Askofu DMZV. Zoezi la uchaguzi limeongozwa na Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Daktari ALEX GEHAZ MALASUSA. Aidha, Askofu Daktari Alex Malasusa amehimiza mshikamano, umoja ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa mujibu wa katiba ya Kanisa. Kaimu Katibu Mkuu wa Dayosisi Ndugu. Joshua Kyelekule ameeleza kuwa, zoezi zima la uchaguzi limefanyika kwa kuzingatia Katiba ya Dayosisi. Mchanganuo wa Matokeo ya Uchaguzi ni kama ifuatavyo: Jumla ya Wapiga kura =222. 1.Mchungaji Stephano Ling'hwa kura =165 2.Mchungaji Mimi brown Kura =57