WARSHA YA WASIMAMIZI TAASISI ZA KKKT NCHINI

Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Alex Gehazi Malasusa amewataka Wakurugenzi wa Taasisi za Kanisa kuwa wabunifu katika kuendesha Taasisi hizo pamoja na kujifunza kwa wengine ili kuongeza ufananisi na kuweza kufanya vizuri katika kutoa huduma bora kwenye jamii. Askofu Dkt. Malasusa ameyasema hayo akiwa jijini Mwanza jumatatu ya tarehe 18/11/2024 wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya Wakuu wa Taasisi za Kanisa zikiwemo Hospitali, Shule, Hotel, Bank, vyombo vya Habari pamoja na Vyuo vinavyomilikiwa na KKKT.