ZIARA YA SIKU 14 WATUMISHI 35 NCHINI UJERUMANI

Kundi la watumishi thelathini na tano 35 kutoka Sharika saba 7 za Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria na Chuo cha Biblia cha Kilutheri Nyakato wanaotekeleza mradi wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi (CCAP) Church Climate Action Partnership kwa kushirikiana na sharika saba 7 na Chuo cha Mission Academy kutoka Ujerumani wamewasili nchini Ujerumani kwa ajili ya kuanza ziara ya siku 14 katika maeneo mbalimbali Kaskazini mwa Ujerumani. #Climate_Partnership