KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 28 2540674
Barua pepe: info@elvd.net
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 28 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza na Geita na kwingineko.
Uongozi wa KKKT-DMZV unatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:
NAFASI ZA KAZI: Mhasibu Msaidizi
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: 2 (Mbili)
MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu – DMZV & Jimbo la Magharibi (Geita)
ATARIPOTI KWA: Mtunza Hazina KKKT-DMZV
WAJIBU WA MHASIBU MSAIDIZI:
· Kupokea na kuingiza takwimu katika mfumo wa kiuhasibu kwa kufuata taratibu za fedha za Dayosisi.
· Kuandaa taarifa ya kazi ya jimbo kila baada ya miezi mitatu na kuiwasilisha Ofisi Kuu ya Dayosisi.
· Kutunza petty cash, risiti, na cheque kwa kufuata taratibu zilizowekwa
· Kuandaa cheque, statement, ntaraka za kutoa na kupokea fedha kwa usahihi.
· Kufanya mlinganisho wa bank (bank reconciliation)
· Kufanya uchambuzi wa hesabu za vitabu na kuwasilisha kwa mtunza hazina.
· Kutoa maelezo yanayotakiwa kwa mujibu wa hoja za wakaguzi.
· Kusaidia mchakato wa kutengeneza bajeti
· Kufanya kazi zingine zitakazopangwa na msimamizi wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Shahada ya kwanza ya Uhasibu kutoka kwenye chuo kinachotambulika na serikali
· Awe Mkristo Mlutheri
· Moyo wa kutumika Kanisani
· Uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika kazi.
· Ujuzi wa kutumia kompyuta (word, power point, excel & Accounting Software – Quick Books)
· Uzoefu katika uandaaji wa akaunti na ujuzi wa hesabu (account preparation & balance sheet)
· Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja.
· Umri kuanzia miaka 23 hadi 45
v NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye sifa watume Barua za Maombi ya Kazi, Wasifu (CV), Vivuli vya Vyeti (Certified Certificate) na Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini/Mahali anapo abudu kwa:
KATIBU MKUU,
KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA
S.L.P 423
NB: Maombi Yatumwe kwa Barua Pepe: elctelvd84@gmail.com
TAREHE YA TANGAZO: 13/07/2024
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 04/08/2024 SAA: 08:00 Mchana
ü KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.