employment vacancy

on 7th October 2022 by elct

news article

 

 

KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria

S.L.P 423 Mwanza

Tel/Fax + 255 28 2540674                                                  

Barua pepe: info@elvd.net

Tovuti: www.elct-elvd.org

Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 26 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.

DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.

DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watuwotekatika mikoa ya Mwanza na Geita na kwingineko.

Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria (KKKT-DMZV) inatoa huduma ya mtoto kwa kushirikiana na Mshirika Mwenza Compassion International Tanzania(CIT). Pia KKKT-DMZV inamiliki shamba lenye ukubwa wa ekari 1000 katika wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza. Uongozi wa Dayosisi unatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:

1.      KAZI: MRATIBU WA KITUO CHA HUDUMA YA MTOTO (1)

MAHALI PA KAZI:Usharika wa Nazareth Katoro

ATARIPOTI KWA: Mchungaji Kiongozi wa Usharika

ATAWAJIBIKA KWA: Katibu Mkuu KKKT – DMZV

WAJIBU WA MRATIBU KITUO CHA HUDUMA YA MTOTO:

·         Kuandaa mpango na bajeti ya Huduma ya Mtoto kwa kushirikiana na watendakazi wengine wa Huduma ya Mtoto kwa uthibitisho na kuithinishwa na uongozi wa Kanisa

·         Kusimamia na kuratibu shughuli zote za wafanyakazi wengine wa kituo ch Huduma ya Mtoto

·         Kuwasilisha ripoti kwa kamati ya uongozi wa Kanisa na Compassion International Tanzania kama itakavyotakiwa kwa pande zote husika

·         Kuhakikisha kuwa taarifa zote za fedha za Watoto zinatunzwa vizuri na kuboreshwa kila mara katika kituo cha Huduma ya Mtoto

·         Kusimamia na kuwa mwangalizi mkuu wa utekelezaji wa mitaala yote inayotumika kituoni msimamizi wa shughuli zote za ufundishwaji wa waalimu wote

·         Kuwajibika kuandaa na kuandika maandiko mbalimbali (proposal) kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya Watoto, wazazi na kituo kwa ujumla

·         Kuhakikisha uwepo wa miundo mbinu inayohitajika kwa Watoto/vijana kujifunza kituoni inapatikana kwa njia ya uhamasishaji wa rasilimali zilizopo na kutafuta njia mbadala za kupata miundo mbinu kwa ajili ya Watoto/vijana

·         Kutathimini maendeleo ya watendakazi wengine wa Huduma ya Mtoto wa kuwasilisha maoni yake kwa kiongozi wa usharika

·         Kusimamia maono, vithaminisho vyote vya msingi vya Huduma kwa wakati wote

·         Kufanya kazi zingine zitakazopangwa na mwajiri

SIFA ZA MWOMBAJI:

·         Shahada ya kwanza ya maendeleo ya jamii, Shahada ya mipango na usimamizi wa miradi au elimu inayohusiana na maeneo hayo.

·         Uwezo mzuri wa kutumia komputa

·         Ujuzi katika kuandaa ripoti ya kazi

·         Mkristo na mwenye moyo wa kutumika kanisani na kuwapenda watoto

·         Uzoefu usiopungua angalau mwaka mmoja katika fani ya maendeleo ya jamii.

·         Mchapakazi mbunifu na mwenye uwezo wa kufanya kazi katika mazingira magumu

 

·         Uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja1.     

NAFASI YA KAZI:Mhasibu Msaidizi (1)

MAHALI PA KAZI:Ofisi Kuu - DMZV

ATARIPOTI KWA:Mtunza Hazina KKKT-DMZV

WAJIBU WA MHASIBU MSAIDIZI:

·         Kupokea na kuingiza takwimu katika mfumo wa kiuhasibu kwa kufuata taratibu za fedha za Dayosisi.

·         Kuandaa taarifa ya kazi ya jimbo kila baada ya miezi mitatu na kuiwasilisha Ofisi kuu ya Dayosisi kwa.

·         Kutunza petty cash, risiti, na cheque kwa kufuata taratibu zilizowekwa

·         Kuandaa cheque, statement, ntaraka za kutoa na kupokea fedha kwa usahihi.

·         Kufanya mlinganisho wa bank (bank reconciliation)

·         Kufanya uchambuzi wa hesabu za vitabu na kuwasilisha kwa mtunza hazina.

·         Kutoa maelrzo yanayotakiwa kwa mujibu wa hoja za wakaguzi.

·         Kusaidia mchakato wa kutengeneza bajeti

·         Kufanya kazi zingine utakazopangiwa na Mkuu wako wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI:

·         Shahada/stashahada ya kwanza ya uhasibu kutoka kwenye chuo kinachotambulika na serikali

·         kozi ya angalau mwaka mmoja kwenye mambo ya uhasibu/manunuzi/biashara n.k

·         Moyo wa kutumika kanisani, aliyeokoka na mwenye maisha ya ushuhuda ya kila siku.

·         Uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika kazi.

·         Ujuzi wa kutumia kompyuta (word power point, excel & Accounting Software – Quick Books)

·          Uzoefu katika uandaaji wa akaunti na ujuzi wa hesabu (account preparation & balance sheet)

·         Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi Zaidi ya moja.

 

2.      NAFASI YA KAZI:Meneja wa Shamba (1)

MAHALI PA KAZI:Shamba la Malya - Kwimba

ATARIPOTI KWA:Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji

WAJIBU WA MENEJA WA SHAMBA:

·         Kuandaa mpango na ratiba za kilimo, kupanda na kuvuna

·         Kusimamia na kuwahikisha kuwa watumishi wote katika shamba wana uelewa wa ratiba za kazi

·         Kuhakikisha kuwa mbegu, mbolea, dawa za kuulia wadudu na vifaa muhimu vya shamba vinapatikana kwa wakati na kutunzwa vizuri

·         Kusimamia na kutunza shamba na mali zilizo katika shamba

·         Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea

·         Kukusanya takwimu za bei na mazao ya shamba

·         Kuandaa taarifa ya utekelezaji katika shamba ya miezi mitztu na kuiwasilisha kwa mkuu wa Idara ya mipango na uwekezaji

·         Kuhakikisha kuwa uzalishaji wa mazao kwenye kitalu (greenhouse) unafanyika muda wote

·         Kutafuta masoko ya bidhaa za shamba na kuhakikisha mazao yanafika sokoni kwa wakati

·         Kufanya kazi zingine utakazopangiwa na Mkuu wako wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI:

  • ·         Shahada/stashahada ya kwanza ya kilimoau shahada ya Sayansi aliyejiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka kwenye chuo kinachotambulika na serikali

·         Uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika kazi.

·         Ujuzi wa kutumia kompyuta (word, Excel)

·          Umri usiozidi miaka 45

·         Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi Zaidi ya moja.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:

Waombaji wenye sifa watume maombi yao kwa:

KATIBU MKUU,

KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA

S.L.P 423

AU KWA BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com

TAREHE YA TANGAZO: 06/10/2022

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 13/10/20222                   SAA: 08:00 Mchana

ü  KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.

 

 

 

 

 

 

Mission Statement

ELVD endeavours to spread the gospel of Jesus Christ, through word and deed, to serve all people in the regions of Mwanza, Geita regions.

UPCOMING EVENTS

Dec 3

Maafali ya 11 ya wanafunzi katika chuo cha biblia cha kilutheri Dayosisi mashariki ya ziwa Victoria

Saturday 12:10 PM

Details →

Oct 5

Mkutano wa LMC-Lutheran Mission Cooperation

Wednesday 08:30 AM

Details →