NAFASI YA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 28 2540674
Barua pepe: info@elvd.net
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 27 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza Geita na kwingineko.
Uongozi wa Dayosisi Mashariki ya Ziwa Viktoria unatangaza nafasi moja ya kazi kwa watu wenye sifa na vigezo kama vilivyo ainishwa hapa chini:
NAFASI YA KAZI: Mhasibu
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu KKKT-DMZV Makongoro Road, Ilemela- Mwanza
ATARIPOTI KWA: Mkuu wa Idara ya Fedha KKKT-DMZV
WAJIBU WA MHASIBU:
· Kupokea na kuingiza takwimu katika mfumo wa kiuhasibu kwa kufuata taratibu za fedha za Dayosisi.
· Kuandaa taarifa ya fedha
· Kutunza petty cash, risiti, na cheque kwa kufuata taratibu zilizowekwa
· Kuandaa cheque, statement, ntaraka za kutoa na kupokea fedha kwa usahihi.
· Kufanya mlinganisho wa bank (bank reconciliation)
· Kufanya uchambuzi wa hesabu za vitabu na kuwasilisha kwa mtunza hazina.
· Kutoa maelezo yanayotakiwa kwa mujibu wa hoja za wakaguzi.
· Kusaidia mchakato wa kutengeneza bajeti
· Kuhakikisha makato yote ya kisheria yanawasilishwa katika mamlaka husika kwa wakati (NSSF,PAYE,Withholding Tax)
· Kufanya kazi zingine zitakazopangwa na Msimamizi wa kazi
SIFA ZA MWOMBAJI WA NAFASI YA KAZI:
· Shahada ya kwanza ya Uhasibu/Accounting kutoka kwenye chuo kinachotambulika na serikali
· Awe Mkristo (Mlutheri)
· Moyo wa kutumika Kanisani
· Uzoefu usiopungua miaka miwili (2) katika kazi.
· Ujuzi wa kutumia kompyuta (word, power point, excel & Accounting Software – Quick Books)
· Uzoefu katika uandaaji wa akaunti na ujuzi wa hesabu (Account Preparation & Balance Sheet)
· Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja.
v NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye sifa watume Barua za Maombi ya Kazi, Wasifu (CV), Vivuli vya Vyeti na Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini/Mahali anapo abudu kupitia Baua Pepe:
BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com
NB: Maombi yatakayotumwa/kuwasilishwa kwa njia tofauti na Barua Pepe tajwa hapo juu HAYATAPOKELEWA!
TAREHE YA TANGAZO: 06/11/2024
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: Ijumaa 22/11/024 SAA: 08:00 Mchana
ü KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.