NAFASI ZA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 28 2540674
Barua pepe: info@elct-elvd.org
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 26 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza na Geita na kwingineko. Uongozi wa Dayosisi unatangaza nafasi za kazi mbili (2) kwa nafasi ya Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji na Afisa manunuzi kama ifuatavyo:
1. KAZI: MKUU WA IDARA YA MIPANGO NA UWEKEZAJI (1)
MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu – KKKT-DMZV
ATARIPOTI KWA: Katibu Mkuu – KKKT-DMZV
WAJIBU WA MKUU WA IDARA YA MIPANGO NA UWEKEZAJI:
· Kusaidia na kuratibu uandaaji wa mpango kazi wa mwaka kwa kila idara
· Kusimamia mchakato wa uandaaji wa mpango mkakati wa Dayosisi
· Kusimamia watumishi walio chini yake ndani ya idara ya mipango na uwekezaji
· Kuratibu uandaaji wa maandiko ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya Dayosisi
· Kutoa picha kamili ya uchumi na mipango ya maendeleo ya Dayosisi kwa muda mfupi na mrefu
· Kubuni na kufanya usimamizi wa miradi ya uwekezaji ya Dayosisi
· Kufanya kazi zingine zitakazopangwa na mwajiri
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Shahada ya kwanza ya Mipango na Usimamizi wa Miradi, Maendeleo ya jamii, Uchumi au elimu inayohusiana na maeneo hayo.
· Uwezo mzuri wa kutumia komputa
· Ujuzi katika kuandaa ripoti ya kazi
· Mkristo (Mlutheri) na mwenye moyo wa kutumika kanisani na kuwapenda watoto
· Uzoefu usiopungua angalau mwaka mmoja katika fani ya usimamizi wa miradi/maendeleo ya jamii.
· Mchapakazi mbunifu na mwenye uwezo wa kufanya kazi katika mazingira magumu
· Uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja
2. NAFASI YA KAZI: AFISA MANUNUZI NA UGAVI (1)
MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu - DMZV
ATARIPOTI KWA: KATIBU MKUU KKKT-DMZV
WAJIBU WA AFISA MANUNUZI NA UGAVI:
· Kuandaa mango wa manunuzi kwa kila mwaka
· Kushauri uongozi juu ya masuala yanayohusiana na manunuzi ya bidhaa/mali za taasisi
· Kuhakikisha kuwa taasisi inafuata taratibu na sera za manunuzi za DMZV na miradi
· Kununua, kuhifadhi na kusimamia usambazaji vifaa na huduma mbaimbali ili kukidhi mahitaji na huduma zinazotolewa katika taasisi
· Kutunza na kuboresha kumbukumbu ya vifaa na mali za ofisi
· Kuratibu vikao vya kamati ya manunuzi kwa mujibu wa sera ya manunuzi DMZV
· Kuandaa hati za kupokelea vifaa
· Kufungua na kutunza ‘Bin Card”
· Kufanya kazi zingine zinazopangwa na msimamizi/mwajiri
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Shahada ya kwanza katika fani ya Ununuzi na Ugavi katika chuo kinachotambulika na serikali
· Uzoefu wa kazi angalau mwaka mmoja (1)
· Ambaye amesajiliwa PSPTB atapewa kipaumbele zaidi
· Ujuzi wa kutumia kompyuta
· Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi Zaidi ya moja.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye sifa watume Barua za maombi, vivuli vya vyeti na barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini kwa:
KATIBU MKUU,
KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA
S.L.P 423
AU KWA BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com
TAREHE YA TANGAZO: 06/12/2022
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 27/12/20222 SAA: 08:00 Mchana
ü KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.