IBADA YA KUINGIZWA KAZINI WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU

Wajumbe Teuliwa wa Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria wameingizwa kazini rasmi na Mhe. Baba Askofu Andrew Petro Gulle Mkuu wa KKKT-DMZV katika Ibada ya Siku ya Bwana ya 13 ya Utatu Jumapili tarehe 03/09/2023 katika Kanisa la KKKT-Imani Kanisa Kuu. Wajumbe wa Halmashauri Kuu wamekabidhiwa Katiba ya Dayosisi na kuweka sahihi katika nyaraka inayoainisha Tamko la kuridhia wajibu wao. #Wajibu Mwema Watoka Kwako!