IBADA YA UBARIKIO DARASA LA KIPAIMARA

Mhe. Baba Askofu Andrew Petro Gulle Mkuu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ameshiriki ibada ya kuwabariki watoto 36 wa darasa la kipaimara Jumapili Tarehe 12/11/2023 katika Kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer - Pasiansi. Mhe. Baba Askofu amewataka watoto hao kuendelea kumcha Mungu kwa uaminifu, kuyakumbuka na kuyaishi mafundisho waliyopata kutoka kwa walimu wao. Ufunuo wa Yohana 3:11-12 ni neno ambalo Mhe. Baba Askofu amewaachia watoto "naja upesi, shika sana ulichonacho, asije mtu akaitwaa taji yako".