Kituo cha Ushauri wa Kisaikolojia

Kitengo cha Ushauri wa Kisaikolojia kinamilikiwa na KKKT – DMZV. Kitengo kipo eneo la National Nyakato karibu na chuo cha VETA Mwanza. Kitengo kina wataalam katika fani ya Ushauri na Saikolojia wenye uwezo wa kutoa mafunzo mbalimbali, ushauri nasihi na matibabu ya kisaikolojia kwa mtu, familia na taasisi bila kujali tofauti za kidini, jinsi, umri, rangi, elimu nk. Lengo ni kuleta ustawi wa afya ya akili kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa kuwajengea uwezo ili kubaini changamoto walizonazo na kupata njia sahihi ya kutatua changamoto hizo kwa ufanisi na kuweza kusonga mbele. Mifano ya shida za Kisaikolojia 1. Depression (Mfadhaiko) 2. Panic disorder (Hofu kubwa) 3. Generalized anxiety disorder (kuwaza sana) 4. Alcohol and Drugs addiction (ulevi wa kupindukia na wa madawa ya kulevya) 5. Post-Traumatic Stress Disorder (kuathirika na tukio)