KKKT-MARATHON 2025 YAFANA

Katika Maadhimisho ya miaka 62 ya Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania Katibu Mkuu wa KKKT-DMZV Bw. Joshua Kyelekule amepokea cheti cha ushiriki wa KKKT - Marathon kwa niaba ya Askofu wa KKKT-DMZV kilichotolewa na mwakilishi wa Mgeni Rasmi Mh. Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Baadhi ya Wachungaji, Watumishi wa Ofisi - Kuu na Wakristo walei kutoka Dayosisi Mashariki ya ziwa Viktoria wameshiriki mbio zikiwa na kwa Lengo la kukusanya fedha za kuwasaidia watoto walemavu na wenye mahitaji maalumu. #KIMBIA KWA MOYO! SAIDIA KWA UPENDO!