MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE

Mradi wa USAID Kizazi Hodari kanda ya Ziwa mkoani Mwanza umeratibu maadhimisho ya Siku ya Mwanamke kanda ya ziwa mkoani mwanza tarehe 04/03/2024 katika Ofisi za Kizazi Hodari Capripoint jijini Mwanza. Maadhimisho haya yameambatana na shughuli mbalimbali kama vile matembezi ya hisani alfajiri, ibada ya pamoja ya asubuhi, kutembelea na kugawa vitu vya mahitaji mbalimbali katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana. Aidha, maadhimisho haya yamehudhuriwa na Asasi zinazotekeleza mradi huu ndani ya mkoa wa mwanza ambazo ni Evangelical Lutheran Church of Tanzania- East of Lake Victoria Diocese (ELCT-ELVD) na Mwanza Outreach care and Support Organization (MOCSO)