MHAFALI YA 14 YA CHUO CHA BIBLIA CHA KILUTHERI NYAKATO - MWANZA YAFANYIKA,WAHITIMU 41 WAASWA KUZINGATIA MAADILI Mahafali ya 14 ya chuo Cha kilutheri Nyakato - Mwanza yamefanyika Jumamosi hii jijini Mwanza yakihusisha wanafunzi 9 wa Diploma ya Theolojia ,Certificate ya Theolojia 21 ,Wainjilisti 7 na Parishworkers 4. Mgeni Rasmi katika mahafali hayo Askofu Mushendwa kutoka Dayosisi ya Magharibi Kigoma na Mwenyeji wake Mkuu wa chuo cha Biblia Cha Kilutheri Nyakato Askofu Oscar Itael Lema ambaye ni Askofu wa Dayosisi Mashariki ya ziwa Viktoria Wageni wengine waliohudhuria Mahafali hayo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Iringa-Prof Edward Hoseah, Makamu Mkuu wa chuo Nyakato Mchg. Mimii Brown, Mwenyekiti wa Bodi ya chuo Dr. Emmanuel Lwankomezi pamoja na Katibu Mkuu wa DMZV Joshua Kyelekule. Na hizi ni picha za matukio mbalimbali za mahafali