IMANI KANISA KUU,JIMBO LA MWANZA KUSINI NA MAGHARIBI WAFANYA VIZURI MASHINDANO YA UIMBAJI DAYOSISI. Mashindano ya uimbaji ngazi ya Dayosisi yaliyofanyika jumapili tarehe 19/10/2025 katika usharika wa Ebenezer Pasiansi huku mgeni rasmi akiwa ni Msaidizi wa Askofu Dean Stephen Ling'hwa John. Katika mashindano hayo yaliyohusisha kwaya mbalimbali kutoka Majimbo yote ya Dayosisi Mashariki ya ziwa Victoria ambapo kwa upande wa vijana kulikuwa na Kwaya 6 na washindi ni kama Ifuatavyo: 1. Vijana imani kanisa Kuu 2. Sayuni Mwatulole - Jimbo la Magharibi 3. Galilaya Buhongwa - Mwanza kusini Na kwa upande kwa Kwaya za MCHANGANYIKO kulikuwa na jumla ya kwaya 13 zilizoshiriki na washindi ni kama Ifuatavyo: 1. Kwaya ya Imani - Imani Kanisa Kuu 2. Kwaya Kuu Galilaya Buhongwa - Jimbo la Mwanza kusini 3. Kwaya Kuu Yesrusalem Kanyerere - Jimbo la Mwanza kusini . Washindi WA kwanza Hadi wa tatu wamejinyakulia zawadi ya Pesa ,cheti pamoja na makombe huku Msaidizi wa Askofu Dean Stephen Ling'hwa John akiwapongeza washiriki wote wa mashindano hayo na kuahidi kuongeza zawadi zaidi kwa watakaofanya vizuri mashindano yajayo.