Baadhi ya matukio katika picha Ibada inayoongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa ya kuwekwa wakfu Askofu wa nne wa KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria (Mwanza). Askofu Dkt. Godson Abel Mollel (KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati, Arusha) akihubiri katika Ibada hiyo amemtaka Askofu Mteule Mchg. Lema kutofanya kazi peke yake pamoja na msaidizi wake bali watende kazi pamoja na Mungu. Ameongeza kuwa hawapaswi kuwa na woga kwa kuwa Mungu yu pamoja nao na kuwabariki wakifanya kazi hiyo kwa kumtanguliza Yeye (Mungu). Askofu Dkt. Mollel amewataka pia wakristo kutii sauti ya Mungu na kufanya kazi kwa bidi kwani kwa kufanya hivyo Mungu atabariki nyumba zao.