MILIONI HAMSINI NA NANE ZAPATIKANA KWAAJILI YA KUPAUWA JENGO LA KANISA

MILIONI HAMSINI NA NANE ZA PATIKANA KWAAJILI YA KUPAUWA JENGO LA KANISA Baba Askofu Oscar I. Lema amezindua rasmi Usharika wa Makedonia-Kishiri leo machi 29, katika ibada ya saa 2:00 asubuhi Askofu Lema amesema Dayosisi inazidi kufanya Uwekezaji katika vituo vyetu vya Dayosisi ambavyo ni kituo cha Afya Nyakato kwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa na kufanya maboresho katika chumba cha upasuaji kwa vifaa bora na vya kisasa na kituo kingine ni shule ya Mwanza Lutheran Secondary School inayota elimu bora kwa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Katika ibada hii kumefanyika harambee kwaajili ya kuwezesha shughuli za upauwaji wa jengo la kanisa ambao makadirio ya gharama ni milioni sabini (70,000,000/=), kupitia harambee hii iliofanyika leo zimekusanywa fedha kiasi cha shilingi milioni hamsini na nane laki tatu hamsini na mbili (58,352,000) ahadi na fedha taslimu Pia mara baada ya ibada kumefanyika zoezi la upandaji miti lililofanywa na viongozi mbali mbali wa Dayosisi pamoja na Mgeni maalumu aliealikwa katika ibada hii ya uzinduzi wa Usharika Bwana Fred Shoo