Mradi wa utunzaji wa mazingira (CCAP) umehitimishwa rasmi Aprili 27, 2026 katika kikao cha mwisho kilichofanyika kimtandao Charming Bungalow Hotel kwa kushirikiana na chama cha kimisioni cha ZMOe cha Ujerumani Kaskazini. Katika kikao hiki waratibu waliweza kuwasilisha kazi zilizotekelezwa na Action Teams 8 katika kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji (2023-2026).Katika kipindi chote mafanikio makubwa yameonekana kwenye upandaji wa miti ya Mbao, kivuli na matunda, ujenzi wa majiko sanifu, uwekaji wa mifumo ya nishati mbadala na uvunaji maji, ufugaji bora wa nyuki,mijadala ya mabadiliko ya tabianchi, uchimbaji & marekebisho ya visima vya maji, elimu kwa jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi, njia bora ya ushirikiano na teknolojia katika dunia ya sasa. Pande zote zilishoshiriki katika mradi huu zinategemewa kuendeleza jitihada hizi katika sharika na taasisi zao ili kuendelea kuchochea mapambano ya mabadiliko ya Tabianchi katika maeneo yao.