PASAKA FESTIVAL 2025

Idara ya Jinsia na Maendeleo Kitengo cha Vijana KKKT - Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria imeadhimisha Tamasha la Pasaka Festival likiwa na lengo maalumu la Kuombea Amani ya Taifa na kukabidhi mikononi mwa Mungu zoezi la Uchaguzi 2025. Zaidi ya Kwaya 19 kutoka Mwanza, Simiyu, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Katoro zimeshiriki pamoja uimbaji wa nyimbo. Waimbaji wakubwa Rose Muhando, Christina Shusho na Bony Mwaitege wamehubiri kwa njia ya uimbaji na kutoa burudani katika tamasha Hilo. Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC) Mhe. Masanja Kungu Kadogosa amewaomba viongozi wa Dini nchini kuhamasisha Amani ya Taifa la Tanzania ikiwa ni pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania