SEMINA YA WAHASIBU WOTE KKKT-DMZV

Idara ya Fedha KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria imefanikiwa kuandaa na kufanya semina ya muda wa siku tatu (3) katika Chuo cha biblia na Theolojia Nyakato kwa lengo la kuwakutanisha watumishi wote wa kada ya uhasibu (Waajiriwa na watumishi wa kujitolea) kufahamiana, kukumbushana kuhusu taratibu na miongozo mbalimbali ya fedha, kupeana uzoefu wa namna ya utendaji kazi katika vituo tofauti ndani ya Dayosisi, kutatua changamoto zinazojitokeza katika utendaji kazi na kuweka mpango na makubaliano ya pamoja ya namna nzuri ya kuboresha utendaji kazi. Semina hii imefunguliwa na Mhe. Baba Askofu Andrew Petro Gulle Mkuu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria. Mhe. Baba Askofu amewahimiza watumishi kuwa waaminifu katika kutekeleza majukumu yao na dhamana kubwa waliyopewa ya kutunza fedha za Kanisa.