UFUNGUZI WA KAMBI YA ETE Baba Askofu wa KKKT-DMZV Oscar I. Lema afungua (semina) kambi ya ETE leo machi 30 ambayo itafanyika kwa siku tatu katika Shule ya Kassa Charitty Pre & Primary School iliyopo Kanyama-Kisesa. Askofu Lema amewaasa wanafunzi wa ETE kuwa semina hii sio tuu ya kitaaluma bali ni safari ya kukua kiroho kwa kujifunza na kuongeza maarifa Wanafunzi wa darasa la ETE wamepata nafasi ya kujifunza juu ya maswala ya Mahubiri yaliyofundishwa na Dean Stephen Ling'hwa John Msaidizi wa Askofu KKKT-DMZV, Uongozi na Utawala Katika Kanisa amefundisha Mchg. Philbert Celestine Mchungaji kiongozi Usharika wa Inuka-Mkuyuni na nyimbo za kitabu cha Tumwabudu Mungu Wetu amefundisha Mwl. Martha Mushi Mratibu wa Muziki Dayosisi. Semina hii imehudhuriwa na wanafunzi 79 kutoka Majimbo matano yaliyo ndani ya Jiji la Mwanza ambayo ni Jimbo la Mwanza Mashariki, Jimbo la Mwanza Kati, Jimbo la Mwanza Kusini, Jimbo la Kaskazini na Imani Kanisa Kuu/Ofisi Kuu