UZINDUZI WA MRADI WA UWAKILI JUNE 2023

Mradi wa miaka mitatu (3) 2023 hadi 2025. Dayosisi 6 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ikiwepo Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria zinahusika katika utekelezaji wa mradi huu. Wawakilishi wa kila Dayosisi sita (6) zinazotekeleza mradi huu zimeshiriki katika uzinduzi wa mradi huu ikiwa ni pamoja na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela. Viongozi (Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Mhe. Baba Askofu Andrew Petro Gulle Mkuu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria) wakipanda miti kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.