Katika siku ya pili wageni kutoka Ujerumani wakiwa na wenyeji wao kupitia utekelezaji wa mradi wa mazingira CCAP walipata fursa ya kusali siku ya jumapili tarehe 18.01.2026 katika ibada ya pili Usharika wa KKKT- Imani Kanisa Kuu na baada ya ibada waliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza kujionea vivutio vya Kigeni na kihistoria. Wageni walitembelea Gunzert House (Nyumba ya kijerumani), Ghalo Tree (mti wa Ghalo), Jiwe la Bismarck,Jiwe Kuu kujionea Mandhari nzuri ya Ziwa Viktoria na Jiji la Mwanza kwa Ujumla