WAJUMBE HALMASHAURI YA MIPANGO NA UWEKEZAJI KKKT-DMZV WAFANYA ZIARA KATIKA SHAMBA LA MALYA-KWIMBA

Halmashauri ya Mipango na Uwekezaji KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ikiongozwa na Mwenyekiti Bi. Alice Moses imefanya ziara katika shamba la Malya llinalomilikiwa na Dayosisi lililopo eneo la Ngudu wilayani Kwimba. ziara hii imefanyika siku ya Jumamosi tarehe 01/06/2024 kwa lengo la kukagua na kujua hali halisi ya shughuli na miradi inayofanyika katika eneo la shamba lenye ukubwa wa ekari 1000. Miradi inayotekelezwa katika shamba ni kama ifuatavyo: 1. Kilimo cha Umwagiliaji 2. Mradi wa Tofali 3. Green House 4. Mradi wa Shule (Proposed Malya Lutheran Secondary School) Mbali na ziara hiyo, Halmshauri ya Mipango na uwekezaji walipata nafasi ya kufanya kikao cha pamoja kujadili taarifa ya maendeleo ya shamba na kuweka mikakati, maazimio na mapatano ya kutekeleza miradi kwa maendeleo na ufanisi zaidi kwa kuzingatia mpango mkakati wa Kanisa wa miaka sita 2024-2029