Washiriki Semina ya Uendelevu na Uwakili wa Maliasili Dayosisi ya Mara, Mwanza na Shinyanga

Mradi wa Uwakili unaofadhiliwa na DANMSSION umetoa mafunzo ya siku tano 5 kwa Dayosisi tatu za Mara, Mwanza na Shinyanga kuhusu Uendelevu na Uwakili wa Maliasili. Mafunzo haya yametolewa kuanzia tarehe 31/07/2023 hadi tarehe 04/08/2023 katika ukumbi wa Charming Bungalow KKKT-Nyakato Mwanza. Mada zilizofundihswa ni pamoja na: Uhifadhi na utunzaji wa rasilimali, Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, Mtazamo wa Kitheolojia katika uhifadhi na utunzaji mazingira, Utatuzi wa migogoro, Utawala Bora, Biblia inasemaje kuhusu utawala Bora, Wajibu wa Kanisa na Viongozi wadini katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira na mwisho kila Dayosisi iliweka mpango kazi wa kushughulikia changamoto ambazo kila Dayosisi inazipa kipaumbele. Shukrani za dhati kwa DANIMSSION katika kufanikisha zoezi hili.