WATU 6 WABATIZWA EMAU RUNZEWE

Mhe. Baba Askofu Andrew Petro Gulle Mkuu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria amewabatiza watu 6. Watu wazima = 3 na Watoto = 3 tarehe 28/12/2023 katika Usharika wa Emau Runzewe Jimbo la Kusini Magharibi. Pia Mhe Baba Askofu amefanya ziara ya kazi ya ufuatiliaji na tathimini ya mradi wa Sinema Leo (chini ya idara ya Misioni na Uinjilisti) inayoendeshwa katika mtaa wa Nyakayenze Usharika wa Emau Runzewe.