ZIARA YA KAZI YA KATIBU MKUU KKKT-DMZV Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria akishirikiana na Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji na Huduma za Jamii leo tarehe 28, Mei wamefanya ziara katika Usharika wa Emanueli-Sengerema ya kukutana na watumishi wa jimbo, usharika na mradi wa ACHIEVE Pamoja na kukagua shughuli za uhitimishaji wa mradi. Pia ziara hii imefika katika Usharika wa Tumaini-Kasamwa kuona shughuli mbalimbali zinazoendelea pamoja na utekelezaji wa mpango mkakati. Vilevile ziara iliendelea mpaka mtaa wa Penueli-Nampalahala kuona na kukagua kazi mbalimbali ikiwemo mpango kazi wa mtaa, uendelevu wa shughuli za mradi wa utunzaji mazingira (CCAP), mradi wa uchimbaji wa visima, mradi wa uwekaji vioo na vigae katika usharikani na mradi wa ufugaji nyuki unaoendelea. Ziara hii imekua na matokeo makubwa sana baada ya vikao vya mrejesho na majadiliano ya namna ya kuboresha kazi hizi za taasisi.