ZIARA YA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU KATIKA SHULE YA MWANZA LUTHERAN SECONDARY

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi kinafanyika kuanzia leo Aprili 29 hadi Aprili 30 katika Ukumbi wa Charming Bungalow-Nyakato. Lengo la kikao hiki ni kupitia taarifa ya fedha januari-disemba 2025 na taarifa ya kazi januari-disemba 2025. Kikao hiki kimeambatana na ziara ya kutembelea na kukagua uzio wa shule ya mwanza lutheran secondary iliopo Sinai-Mabatini ili wajumbe wa halmashauri kuu waweze kuona kazi ya ujenzi inayoendelea.