Psychological Counselling

Kitengo cha Ushauri wa Kisaikolojia kinamilikiwa na KKKT – DMZV. Kitengo kipo eneo la National Nyakato karibu na chuo cha VETA Mwanza. Kitengo kina wataalam katika fani ya Ushauri na Saikolojia wenye uwezo wa kutoa mafunzo mbalimbali, ushauri nasihi na matibabu ya kisaikolojia kwa mtu, familia na taasisi bila kujali tofauti za kidini, jinsi, umri, rangi, elimu nk.

 

Lengo ni kuleta ustawi wa afya ya akili kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa kuwajengea uwezo ili kubaini changamoto walizonazo na kupata njia sahihi ya kutatua changamoto hizo kwa ufanisi na kuweza kusonga mbele.

Huduma hii inasaidia katika shida za aina gani?

Mifano ya shida za kawaida

1.      Kutokuelewana baina ya wanandoa

2.      Kutokuelewana baina ya wazazi na mtoto

3.      Kijana kutokujua asome nini

4.      Kuachana na mchuma, mume au mke

5.      Kufiwa na mtu wa karibu

6.      Kujulishwa utambuzi wa ugonjwa kama kansa

7.      Kuwaza sana, kukata tamaa, kutaka kujiua nk.

 

Mifano ya shida za Kisaikolojia 

1.      Depression (Mfadhaiko)

2.      Panic disorder (Hofu kubwa)

3.      Generalized anxiety disorder (kuwaza sana)

4.      Alcohol and Drugs addiction (ulevi wa kupindukia na wa madawa ya kulevya)

5.      Post-Traumatic Stress Disorder (kuathirika na tukio)

 

Utaratibu wa huduma

Utaratibu wa huduma ni kipindi kimoja cha saa nzima kila wiki kwa muda wa wiki kadhaa na hutolewa kwa njia zifuatazo;

1.      Kuzungumza na mteja ana kwa ana (physical session)

2.      Kuzungumza na mteja kwa njia ya mtandao (online session)

 

Masaa ya kazi ni kuanzia Jumatatu – Ijumaa Saa 2.00 asubuhi – 10.00 jioni

Mawasiliano: Simu +255745902089 au +255744934336

UPCOMING EVENTS

Feb 14

Marriage revival 2025

Friday 07:00 AM

Details →

Jan 19

Utambulisho wa Askofu na Msaidizi wa Askofu kwa Prof. Kabudi

Sunday 01:46 PM

Details →