TANGAZO LA KAZI MHASIBU MSAIDIZINAFASI 2

on 28th May 2026 by elct

news article

KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria

S.L.P 423 Mwanza

Tel/Fax + 255 28 2540674

Barua pepe: info@elvd.net Tovuti: www.elct-elvd.org

Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.

DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.

DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza, Geita na kwingineko.

Uongozi wa Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria unatangaza nafasi ya kazi kama ifuatavyo:

 

1. NAFASI YA KAZI: Mhasibu Msaidizi IDADI YA NAFASI YA KAZI: Mbili (2) MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu KKKT-DMZV

ATARIPOTI KWA: Mkuu wa Idara ya Fedha KKKT-DMZV


WAJIBU WA MHASIBU MSAIDIZI:

·       Kuandaa malipo, statement, nyaraka za kutoa na kupokea fedha kwa usahihi

·       Kuhakikisha kuwa malipo yote yanayofanyika yana viambatanisho sahihi na toshelevu

·       Kuhesabu bill za wateja

·       Kutunza mafaili ya nyaraka za malipo/matumizi na mapato kwa mpangilio mzuri na hali ya usafi

·       Kutunza nyaraka za makato ya kisheria kwenye mafaili maalum

·       Kusaidia mchakato wa kutengeneza bajeti

·       Kuandaa Payment Voucher kwa mujibu wa malipo halali

·       Kupokea na kuingiza takwimu katika mfumo wa kiuhasibu kwa kufuata taratibu za Fedha za Dayosisi

·       Kufanya kazi zingine zinazopangwa na msimamizi wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI:

·       Shahada ya kwanza ya Uhasibu kutoka kwenye chuo kinachotambulika na serikali

·       Awe Mkristo Mlutheri

·       Moyo wa kutumika Kanisani

·       Uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika kazi.

·       Ujuzi wa kutumia kompyuta (word, power point, excel & Accounting Software – Quick Books)

·        Uzoefu katika uandaaji wa akaunti na ujuzi wa hesabu (account preparation & balance sheet)

·       Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja.

 

v  NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:

Waombaji wenye Sifa Watume/Kuwasilisha Maombi ya kazi kwa:

KATIBU MKUU KKKT-DMZV

S.L.P 423, MWANZA

Kupitia Barua Pepe: elctelvd84@gmail.com

NB: Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya Barua Pepe

Muombaji wa Nafsi ya kazi atatakiwa kuwasilisha vitu vifuatavyo:

·       Barua ya Maombi ya Kazi,

·       Wasifu/CV

·       Vivuli vya Vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria (Certified Certificates)

·       Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini/Mahali anapo abudu TAREHE YA TANGAZO: 28/05/2026

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 30/06/2026                 SAA: 08:00 Mchana

ü  KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.

Mission Statement

ELVD endeavours to spread the gospel of Jesus Christ, through word and deed, to serve all people in the regions of Mwanza, Geita regions.

UPCOMING EVENTS

Aug 26

DAY TRIP AT SERENGETI NATIONAL PARK

Wednesday 02:45 PM

Details →

Apr 29

HALMASHAURI KUU YA DAYOSISI

Wednesday 03:29 PM

Details →