TANGAZO LA ZABUNI LA UUZAJI WA BOTI YA KKKT-DMZV AINA YA YAMAHA BOW –RIDER MYSTIQUE 190 LENYE RANGI NYEUPE NA NJANO NA GARI AINA YA TOYOTA HILUX SURF YENYE USAJILI NAMBA T 805 AJJ ILIYOPO MWANZA.
Uongozi wa KKKT-DMZV unapenda kuwatangazia na kuwakaribisha wenye nia ya kununua boti tajwa hapo juu, tunakaribisha watu binafsi, mashirika, makampuni, taasisi na vikundi vinavyotimiza vigezo na masharti katika tangazo hili.
1. Zabuni hii itashindanishwa kitaifa (National Competitive)
2. Zabuni hii ya uuzaji wa boti itaanza rasmi tarehe 13/09/2023 Saa 04:00 asubuhi
3. Kabrasha la zabuni linapatikana katika ofisi ya Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi Mashariki ya ziwa Viktoria (DMZV) kwa Tsh 20,000/= pia kwa mwombaji anayehitaji ufafanuzi, maelezo ya ziada kuhusu zabuni hii afike ofisi ya Katibu Mkuu wa KKKT- DMZV saa za kazi kuanzia Saa 03:00 asubuhi hadi Saa 10:00 jioni, Jumatatu – Ijumaa.
4. Maombi yote ya zabuni yawasilishwe na kusajiliwa katika ofisi ya Katibu Mkuu wa KKKT-DMZV kabla ya kudumbukizwa kwenye sanduku la zabuni la Dayosisi.
5.Maombi kwa njia ya Fax, Barua pepe hayatapewa kipaumbele
6. Kwa mnunuzi atakaye hitaji kuona bidhaa hii/hizi awasiliane na JOYGRACE SHOO kwa simu namba +255 764 589 855/0623 850 509 kabla ya tarehe 13/10/2023 saa 10:00 jioni. Muda wa kwenda kukagua mali hii/hizi ni kuanzia Saa 03:00 asubuhi mpaka Saa 10:00 jioni, Jumatatu – Ijumaa.
|
Aina ya bidhaa |
Specification |
Hali |
Mahali ilipo |
1 |
F 130 HP YAMAHA |
Model; 2015 Engine Serial Prefix; 6EM-L Engine Serial Number: 1000465-L |
Nzuri na inafanya kazi |
MWANZA |
2 |
TOYOTA HILUX SURF |
Model: Y-KZN130G-GKPGT Engine No:1KZ-TE 2982CC Frame No. KZN130-9037732 |
Nzuri na inafanya kazi |
MWANZA |
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 11/10/2023 Saa 10:00 jioni. Waombaji /wawakilishi wanaalikwa kuhudhuria ufunguzi wa zabuni hizo utakaofanyika tarehe 13/10/2023 katika ukumbi wa Bethania (Rest House) uliopo Makao makuu ya Dayosisi.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba zifuatazo:
AFISA MIPANGO NA UWEKEZAJI - DMZV.
JOYGRACE SHOO: +255 764 589 855
Barua Pepe; shoojoygrace@gmail.com
KATIBU MKUU- DMZV.
ROGATH LEWIS MOLLEL: +255 713 640 338, +255 767 640 338
Barua Pepe: rogathlewis@yahoo.com au GS@elct-elvd.org