NAFASI ZA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 28 2540674
Barua pepe: info@elvd.net
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 27 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza na Geita na kwingineko.
Taarifa kuhusu Huduma ya Mtoto: Ni huduma inayotolewa na Compassion International Tanzania iliyojikita zaidi katika kumkomboa kijana kutoka katika umaskini kwa jina la Yesu! Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria kwa kushirikiana na mshirika mwenza CIT inatekeleza program hii katika vituo vinne KKKT-Misungwi, Magu, Bugando na Katoro. Uongozi wa KKKT-DMZV unatangaza nafasi za kazi zifuatazo:
1.
N NAFASI YA KAZI: Mhasibu/CYD WORKER CAHIER (1)
MAHALI PA KAZI: Usharika wa KKKT- Nazareth Katoro
ATARIPOTI KWA: Mchungaji Kiongozi wa Usharika
WAJIBU WA CYD WORKER CASHIER/MHASIBU:
· Kuhifadhi fedha za matumizi madogo madogo ya Kituo (Petty Cash) na kuweka kumbukumbu sahihi za matumizi yake na kuandaa hati za malipo ya petty cash yote yanayofanyika katika Huduma ya Mtoto.
· Kuwajibika kufanikisha matokeo yote ya watoto na vijana na viashiria vyake kwa mujibu wa Muongozo wa huduma.
· Kusaidia na kushirikiana na wafanyakazi wengine wa kituo kama inavyohitajika.
· Kushiriki katika kuwatembelea walengwa majumbani mwao ili kujua maendeleo yao kulingana.
· Kuhusika katika ujazaji na kuhuisha taarifa za watoto kwenye mfumo wa connect
· Kuandaa ripoti ya fedha ya kila mwezi na kisha kuiwasilisha kwa Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Vijana.
· Kushiriki katika shughuli za uandishi barua za watoto kutoka na kwenda kwa wafadhili.
· Kuhakikisha kuwa vitabu vyote vya mahesabu vinatunzwa vizuri katika hali bora na ya usalama.
· Kuhusika na uandaaji na utoaji wa hati ya malipo na hundi zote za malipo kwa utaratibu uliowekwa.
· Kuhakikisha kwamba maingizo yote yatokanayo na risiti/ stakabadhi mbalimbali za fedha pamoja na viambatanisho vyake vinawekwa kwenye “fast track” na vinaratibiwa vizuri kila siku.
· Kuandaa na kuwasilisha taarifa ya matumizi ya fedha za Kituo kila mwezi kwenda kwa ngazi husika.
· Kufanya malipo kutokana na uamuzi wa kamati kama ilivyopangwa na kwa mujibu wa sera na kanuni za kifedha za Ushirika-wenza.
· Kutunza fedha za Kituo kwenye akaunti maalumu iliyofunguliwa kwa ajili ya Huduma ya Mtoto katika benki husika.
· Kulipa ada za shule na gharama nyingine za mahitaji yatakayojitokeza kwa mlengwa aliyepo katika programu.
· Kufanya kazi nyinginezo za kiofisi katika kituo kama atakavyopangiwa na Mratibu wa Kituo cha Huduma ya Mtoto, kamati na Uongozi wa kanisa.
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Stashahada/Shahada ya kwanza ya Uhasibu kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali
· Umri kuanzia miaka 23 na si zaidi ya miaka 40
· Uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika kazi.
· Ujuzi wa kutumia kompyuta na mifumo ya kiuhasibu (Word,Power point, Excel & Quick Books etc,)
· Uzoefu katika uandaaji wa akaunti na ujuzi wa hesabu (account preparation & balance sheet)
· Awe Mkristo Mlutheri mwenye moyo wa kuwatumikia watoto/vijana
2. NAFASI ZA KAZI: Mhasibu Msaidizi (2)
MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu – DMZV
ATARIPOTI KWA: Mtunza Hazina KKKT-DMZV
WAJIBU WA MHASIBU MSAIDIZI:
· Kupokea na kuingiza takwimu katika mfumo wa kiuhasibu kwa kufuata taratibu za fedha za Dayosisi.
· Kuandaa taarifa ya kazi ya jimbo kila baada ya miezi mitatu na kuiwasilisha Ofisi Kuu ya Dayosisi.
· Kutunza petty cash, risiti, na cheque kwa kufuata taratibu zilizowekwa
· Kuandaa cheque, statement, ntaraka za kutoa na kupokea fedha kwa usahihi.
· Kufanya mlinganisho wa bank (bank reconciliation)
· Kufanya uchambuzi wa hesabu za vitabu na kuwasilisha kwa mtunza hazina.
· Kutoa maelezo yanayotakiwa kwa mujibu wa hoja za wakaguzi.
· Kusaidia mchakato wa kutengeneza bajeti
· Kufanya kazi zingine utakazopangiwa na Mkuu wako wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Shahada/Stashahada ya kwanza ya uhasibu kutoka kwenye chuo kinachotambulika na serikali
· Awe Mkristo Mlutheri
· Moyo wa kutumika Kanisani
· Uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika kazi.
· Ujuzi wa kutumia kompyuta (word, power point, excel & Accounting Software – Quick Books)
· Uzoefu katika uandaaji wa akaunti na ujuzi wa hesabu (account preparation & balance sheet)
· Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi z aidi ya moja.
v NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye sifa watume Barua za Maombi ya Kazi, Wasifu (CV), Vivuli vya Vyeti na Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini/Mahali anapo abudu kwa:
KATIBU MKUU,
KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA
S.L.P 423
AU KWA BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com
TAREHE YA TANGAZO: 03/06/2024
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 23/06/2024 SAA: 08:00 Mchana
ü KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.