NAFASI YA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 282 540 674
Barua pepe: info@elct-elvd.org
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 27 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza na Geita na kwingineko.
NAFASI YA KAZI: Mratibu wa Elimu na Afya
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu KKKT-DMZV
ATARIPOTI KWA: Mkuu wa Idara ya Huduma za Jamii
WAJIBU WA KAZI:
· Kuandaa na kuratibisha vikao vya kikatiba vya vitengo vya Elimu na Afya katika Dayosisi
· Kubuni njia za uendeshaji wa shule ya Sekondari ya Kilutheri Mwanza na Malya
· Kushauri uongozi juu ya uendeshaji miradi na program za vitengo vya Elimu na Afya
· Kusaidia na kuratibisha usajili wa shule za awali na sekondari DMZV
· Kuratibisha uanzishaji au ufufuaji wa shule za awali au msingi katika sharika
· Kusimamia utekelezaji wa sera na miongozo mbalimbali ya Elimu na Afya na kuhakikisha kuwa sera na miongozo inasambazwa kwa wadau
· Kuratibisha utoaji wa ushauri wa Afya kwa wakristo katika sharika za DMZV na kufuatilia uendeshaji wa vituo vya Afya
· Kuratibisha mradi wa huduma ya mtoto na kijana (compassion) unaotekelezwa katika sharika za DMZV
· Kubuni na kuandaa miradi ya Elimu na Afya katika Dayosisi
· Kusimamia watumishi katika vitengo vya Elimu na Afya katika Dayosisi
· Kufanya kazi zingine zinazopangwa na msimamizi
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Uzoefu katika kazi za huduma za jamii kama vile, Mahusiano ya Umma, Elimu ya Jamii, Uchunguzi wa Afya/Utabibu na maeneo mengine yanayohusiana na maeneo tajwa
· Uzoefu usipungua mwaka mmoja (1) katika nafasi ya uongozi katika taasisi za Elimu/Afya
· Uwezo katika kushughulikia masuala ya afya ya umma
· Mkristo (Mlutheri) na mwenye moyo wa kutumika kanisani
· Uwezo mzuri wa kuandaa ripoti
· Ujuzi na uelewa wa kanuni na misingi ya usimamizi wa program za Elimu na Afya
· Ujuzi wa kutumia kompyuta
· Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi Zaidi ya moja.
SIFA ZA KIELIMU:
· Shahada katika fani ya Elimu, Afya ya Uma, Utabibu, Utawala wa Afya (Degree in Health Administration) au fani zingine zinazohusiana katika chuo kinachotambulika na serikali.
v NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye sifa wawasilishe Barua za maombi ya kazi, wasifu (CV), Vivuli vya Vyeti na Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini kwa:
KATIBU MKUU,
KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA
S.L.P 423.
BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com
TAREHE YA TANGAZO: 16/03/2023
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 05/04/2023 SAA: 08:00 Mchana
NB: Maombi yawasilishwe kwa njia ya barua pepe tu. Na sio vinginevyo
ü KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.