NAFASI YA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 28 2540674
Barua pepe: info@elct-elvd.org
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 27 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza na Geita na kwingineko.
Taarifa kuhusu Charming Bungalow: Ni nyumba za kulala wageni zinazomilikiwa na KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria, zipo Nyakato karibu na kituo cha Afya/Chuo cha Biblia na Theolojia Nyakato KKKT- DMZV. Uongozi wa Dayosisi unatangaza nafasi moja ya kazi kama ifuatavyo:
NAFASI YA KAZI: Mpishi
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: Nyumba za kulala wageni (Charming Bungalow) - Nyakato
ATARIPOTI KWA: Meneja
WAJIBU WA MPISHI:
· Kuwajibika katika kuandaa chakula kwa kuzingatia mahitaji ya mteja/mgeni
· Kuhakisha kuwa chakula na vifaa vyote vya kuandalia chakula vipo katika hali ya usafi na usalama
· Kuandaa na kupanga mpangilio wa vyakula katika hoteli (Menu)
· Kufanya usafi eneo la kuandaa chakuala/jiko na mazingira yanayozunguka
· Kupokea na kushughulikia mahitaji ya chakula ya wageni/wateja
· Kuwasiliana na wafanyakazi wengine katika kuandaa chakula au kufanya maboresho ya kuvutia kwa wateja
· Kubuni mapishi mapya katika hoteli
· Kusimamia na kudumisha mahusiano ya wateja
· Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wengine namna ya kuandaa chakula
· Kupokea maoni kutoka kwa wateja/wageni na kuyafanyia kazi
· Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na msimamizi.
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Cheti cha usimamizi wa hoteli (Hotel Management)
· Mwenye cheti cha mafunzo ya utayarishaji wa vyakula mbalimbali vya asili na kigenikutoka katika chuo kinachotambulika atapewa kipaumbele zaidi
· Uzoefu wa kazi ya upishi katika hoteli au mgahawa/restaurant usiopungua miaka miwili (2) na zaidi
· Uwezo mzuri wa kuhudumia na kuzungumza na wateja kwa ukarimu (good customer care and hospitality)
· Mwenye maadili ya Kikristo
· Mwenye moyo wa kutumika Kanisani
v NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye sifa watume Barua za maombi ya kazi, wasifu (CV), Vivuli vya Vyeti na Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini kwa:
KATIBU MKUU,
KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA
S.L.P 423.
AU KWA BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com
TAREHE YA TANGAZO: 09/03/2023
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 29/03/2023 SAA: 08:00 Mchana
ü KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.