NAFASI ZA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 282 540 674
Barua pepe: info@elct-elvd.org
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 27 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza, Geita na kwingineko.
Taarifa kuhusu Compassion International Tanzania: Ni shirika lililojikita katika kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwatoa watoto katika umaskini wa kiroho, kiuchumi na kimwili. Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria inatoa huduma ya mtoto kwa kushirikiana na Mshirika Mwenza Compassion International Tanzania (CIT) katika vituo vinne. Uongozi wa Dayosisi unatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:
v NAFASI YA KAZI: Child and Youth Development Worker - Accountant
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: KKKT-Yerusalemu Misungwi
ATARIPOTI KWA: Mratibu wa Kituo cha Huduma ya Mtoto na Maendeleo ya Kijana
ATAWAJIBIKA KWA: Mchungaji Kiongozi wa Usharika
WAJIBU WA KAZI:
· kumshuhudia Yesu Kristo kwa uaminifu na kuwa mtetezi wa watoto na vijana.
· Kuweka mpango na kufuatilia mahudhurio na ushiriki wa walengwa kwenye programu zote za kituo cha Maendeleo ya Mtoto.
· Kuwafundisha walengwa uandishi wa barua kwa kutumia mtaala wa barua uliopo, akishirikiana na waalimu.
· Kuhakikisha kuwa kila mlengwa aliyefadhiliwa anaandika barua kwa mfadhili wake kama ilivyopangwa na kwa ubora unachotakiwa kwa mujibu wa mwongozo wa mawasiliano.
· Kuhuisha taarifa kamili za mtoto/kijana kwa wakati na kwa usahihi kulingana na mahitaji ya ofisi ya huduma ya mtoto.
· Kufuatilia hali za ujumla za maendeleo ya walengwa kwa kuwatembelea majumbani na mashuleni mwao na kuchukua/kupendekeza hatua muhimu za kuchukua.
· Kutoa taarifa kwa kamati ya Huduma ya Mtoto, juu ya ubadhilifu wa fedha au tabia isiyoridhisha kwa mmojawapo wa Watendakazi wengine wa Kituo.
· Kuhifadhi fedha za matumizi madogo madogo ya Kituo (Petty Cash) na kuweka kumbukumbu sahihi za matumizi yake na kuandaa hati za malipo ya petty cash yote yanayofanyika katika Huduma ya Mtoto.
· Kuwa miongoni mwa walimu wa walengwa
· Kushiriki kikamilifu ibada ya asubuhi ya watendakazi wote kabla ya kuanza kazi.
· Kuhudhuria na kushiriki vikao vya wazazi.
· Kuhudhuria na kushiriki kikamilifu vikao vya watendakazi kila mwezi au zaidi pale itakapobidi.
· kuwajibika kwenye kufanikisha matokeo yote ya watoto na vijana na viashiria vyake kwa mujibu wa Mwongozo wa huduma.
· Kusaidia na kushirikiana na wafanyakazi wengine wa kituo kama inavyohitajika.
· Kushiriki katika kuwatembelea walengwa majumbani mwao ili kujua maendeleo yao kulingana.
· Kuhusika katika ujazaji na kuhuisha taarifa za watoto kwenye connect
· Kuandaa ripoti ya kazi yake kila mwezi na kisha kuiwasilisha kwa Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na vijana.
· Kushiriki katika shughuli za uandishi barua za watoto kutoka na kwenda kwa wafadhili
· Kuhakikisha kuwa vitabu vyote vya mahesabu vinatunzwa vizuri katika hali bora na ya usalama.
· Kuhusika na uandaaji na utoaji wa hati ya malipo na hundi zote za malipo kwa utaratibu uliowekwa.
· Kuhakikisha kwamba maingizo yote yatokanayo na risiti/ stakabadhi mbalimbali za fedha pamoja na viambatanisho vyake vinawekwa kwenye “fast track” na vinaratibiwa vizuri kila siku.
· Kuandaa na kuwasilisha taarifa ya matumizi ya fedha za Kituo kila mwezi kwenda kwa kwa ngazi husika.
· Kufanya malipo kutokana na uamuzi wa kamati kama ilivyopangwa na kwa mujibu wa sera na kanuni za kifedha za Ushirika-wenza na DMZV.
· Kutunza fedha za Kituo kwenye akaunti maalumu iliyofunguliwa kwa ajili ya Huduma ya Mtoto katika benki husika.
· Kulipa ada za shule na gharama nyingine za mahitaji yatakayojitokeza kwa mlengwa aliyepo katika programu.
· kufanya kazi nyinginezo za kiofisi katika kituo kama atakavyopangiwa na Mratibu wa Kituo cha Huduma ya Mtoto, na Uongozi wa kanisa.
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Uzoefu wa kazi katika fani ya Uhasibu, Maendeleo ya Jamii angalau miaka miwili (2)
· Mkristo Mlutheri mwenye kuishi Maisha ya ushuhuda ya kila siku na wakili wa Watoto/vijana
· Mwenye moyo wa kutumika Kanisani na kuwatumikia Watoto/vijana
· Umri kuanzia miaka 23 na si zaidi ya miaka 40
SIFA ZA KIELIMU:
· Shahada ya Uhasibu kutoka katika chuo kinachotambulika na serikali
· Mwenye Ujuzi kwenye maendeleo ya Jamii, Ualimu, Watoto na kozi angalau ya miaka miwili fani ya uhasibu atapewa kipaumbele
v NAFASI YA KAZI: AFISA MANUNUZI NA UGAVI
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: KKKT- KKKT- Ofisi Kuu (DMZV)
ATARIPOTI KWA: Katibu Mkuu
WAJIBU WA KAZI:
· Kuandaa mpango wa manunuzi kwa kila mwaka
· Kushauri uongozi juu ya masuala yanayohusiana na manunuzi ya bidhaa/mali za taasisi
· Kuhakikisha kuwa taasisi inafuata taratibu na sera za manunuzi za DMZV na miradi
· Kununua, kuhifadhi na kusimamia usambazaji vifaa na huduma mbalimbali ili kukidhi mahitaji na huduma zinazotolewa katika taasisi
· Kutunza na kuboresha kumbukumbu ya vifaa na mali za ofisi
· Kuratibu vikao vya kamati ya manunuzi kwa mujibu wa sera ya manunuzi DMZV
· Kuandaa hati za kupokelea vifaa
· Kufungua na kutunza ‘Bin Card”
· Kuandaa taarifa ya kazi ya miezi mitatu (3) na mpango kazi wa mwaka na kuwasilisha kwa msimamizi wa kazi
· Kufanya kazi zingine zinazopangwa na msimamizi/mwajiri
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Uzoefu wa kazi angalau mwaka mmoja (1)
· Ambaye amesajiliwa PSPTB atapewa kipaumbele zaidi
· Ujuzi wa kutumia kompyuta
· Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi Zaidi ya moja.
· Mkristo Mlutheri mwenye moyo wa kutumika Kanisani
SIFA ZA KIELIMU:
· Shahada ya kwanza katika fani ya Ununuzi na Ugavi katika chuo kinachotambulika na serikali
v NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI:
Waombaji wenye sifa wawasilishe Barua za maombi ya kazi, Wasifu (CV), Vivuli vya Vyeti na Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini kwa:
KATIBU MKUU,
KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA
BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com
TAREHE YA TANGAZO: 31/08/2023
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 19/09/2023 SAA: 08:00 Mchana
NB: Maombi yawasilishwe kwa njia ya barua pepe tu. Na sio vinginevyo
ü KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.