NAFASI ZA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 282 540 674
Barua pepe: info@elct-elvd.org
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 27 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza, Geita na kwingineko.
Uongozi wa Dayosisi unatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:
v NAFASI YA KAZI: Mkaguzi wa Ndani Msaidizi
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: Ofisi Kuu KKKT-DMZV
ATARIPOTI KWA: Mkaguzi wa Ndani DMZV
WAJIBU WA KAZI:
- Kukagua kwa kina vitabu vya fedha kuanzia ngazi ya sharika, vitengo, vituo,majimbo na ofisi kuu
- Kutoa ushauri wa kuboresha utunzaji mali za Dayosisi na kuboresha vyanzo vya mapato ya ndani nan je
- Kufanya ukaguzi wa kushtukiza na wa ratiba wa vituo, majimbo, sharika, miradi nataasisi za dayosisi na kutoa taarifa kwa Mkuu wa Dayosisi
- Kuhimiza matumizi ya fedha katika Hazina Kuu, vituo, majimbo na sharika zitumike kwa kuzingatia makisio yaliyoidhinishwa ipasavyo
- Kukagua uandikaji wa vitabu na kumbukumbu za fedha za siku kwa siku kuona kuwa mambo yote yametunzwa kwa usahihi na usalama
- Kukagua taarifa za vipindi vya miezi mitatu (3) katika sharika, vituo na majimbo
- Kuhakikisha kuwa fedha taslimu zilizo mkononi mwa mhasibu na zilizo benki zinalingana na zilizooneshwa kwenye vitabu vya kumbukumbu za fedha
- Kuhakikisha kuwa urari kila mwezi ni saw ana unafannyika
- Kuhakikisha kuwa mahesabu ya mwisho wa mwaka yametengenezwa na kukamilishwa ipasavyo na kwa wakati unaotakiwakuhudhuria vikao anapohitajika bila kura
- kufanya kazi zingine zitakazopangwa na msimamzi/mwajiri
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Mkristo Mlutheri na mwenye moyo wa kutumika Katika Kanisa
· Sifa za ziada kama vile CPA (T), CA, ACCA au sifa nyingine zinazolingana zinazotolewa na NBAA
· Uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili (2) na kuendelea
· Ujuzi katika matumizi ya Kompyuta na program za kuhifadhi data
· Elimu kuhusu taratibu, sheria na kanuni za ukaguzi wa fedha
SIFA ZA KIELIMU:
· Shahada ya kwanza ya uhasibu au usimamizi wa fedha kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali
v NAFASI YA KAZI: Meneja wa Hoteli
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: Charming Bungalow Hotel- Nyakato
ATARIPOTI KWA: Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji
WAJIBU WA KAZI:
· Kusimamia na kuhakikisha usalama wa eneo la kazi
· Kusimamia wafanyakazi katika Hoteli
· Kubuni njia mbalimbali za uendeshaji wa hoteli
· Kusimamia na kudumisha uhusiano mzuri wa wageni na wateja
· Kusimamia na kufuatilia orodha na mali za hoteli
· Kuandaa, kusimamia na kutengeneza bajeti za uendeshaji wa kituo
· Kufanya tathimini za kawaida za uboreshaji wa Huduma ya wateja
· Kukusanya malipo na kudumisha kumbukumbu za bajeti, fedha na gharama
· Kuandaa ripoti na taarifa ya kazi ya hoteli kila baada ya miezi mitatu na mwaka
· Kushughulikia malamiko na maswali ya wateja ili kukuza biashara
· Kusimamia ufuatiliaji wa taratibu za kisheria za Ncji, Afya, Usalama, mapato na Leseni za Hoteli
· Kuandaa mpango kazi wa kituo, taarifa ya kazi na taarifa ya mapato na matumizi kwa kila mwezi na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji.
· Kupanga, kutekeleza na kusimamia shughuli za kila siku za hoteli
· Kufanya kazi zingine utakazo pangiwa na Msimamizi/Mwajiri
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Cheti cha usimamizi wa hoteli (Hotel Management)
· Uwezo mzuri wa mawasiliano ya kutunza mitandao kama barua pepe, facebook, instagram, twitter na kufanya booking.
· Uwezo mzuri wa kuhudumia na kuzungumza na wateja kwa ukarimu (good customer care and hospitality)
· Uzoefu wa kazi angalau mwaka mmoja na kuendelea katika hoteli zinazotambulika
· Mwenye maadili ya Kikristo
· Mwenye moyo wa kutumika Kanisani
SIFA ZA KIELIMU:
· Stashahada/shahada ya usimamizi wa biashara au fani zingine
v NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye sifa wawasilishe Barua za maombi ya kazi, Wasifu (CV), Vivuli vya Vyeti na Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini kwa:
KATIBU MKUU,
KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA
BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com
TAREHE YA TANGAZO: 01/11/2023
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 20/11/2023 SAA: 08:00 Mchana
NB: Maombi yawasilishwe kwa njia ya barua pepe tu. Na sio vinginevyo
KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.