TANGAZO LA KAZI - MENEJA WA SHAMBA

on 16th March 2025 by elct

news article

NAFASI YA KAZI

KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria       

S.L.P 423 Mwanza

Tel/Fax + 255 28 2540674                                                     

Barua pepe: info@elct-elvd.org

Tovuti: www.elct-elvd.org

Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 27 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.

DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.

DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza, Geita na kwingineko. KKKT-DMZV inamiliki shamba lenye ukubwa wa ekari 1000 katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza. Uongozi wa Dayosisi unatangaza nafasi ya kazi moja (1) kwa nafasi ya Meneja wa Shamba:

NAFASI YA KAZI: Meneja wa Shamba (1)

      MAHALI PA KAZI: Shamba la Malya - Kwimba

      ATARIPOTI KWA: Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji

 

WAJIBU WA MENEJA WA SHAMBA:

·       Kuandaa mpango na ratiba za kilimo, kupanda na kuvuna katika shamba

·       Kusimamia na kuhakikisha kuwa watumishi wote katika shamba wana uelewa wa ratiba za kazi

·       Kuhakikisha kuwa mbegu, mbolea, dawa za kuulia wadudu na vifaa muhimu vya shamba vinapatikana kwa wakati na kutunzwa vizuri

·       Kusimamia na kutunza shamba, mali na miradi iliyopo katika shamba

·       Kupokea na kutunza fedha zinazopatikana kupitia shughuli za shamba na kuhakikisha zinahifadhiwa benki na kuepuka kutumia fedha mbichi

·       Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea

·       Kukusanya takwimu za bei na mazao ya shamba

·       Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya shamba ya kila miezi mitatu 3, mpango kazi wa mwaka na kuiwasilisha kwa mkuu wa Idara ya mipango na uwekezaji

·       Kuhakikisha kuwa uzalishaji wa mazao kwenye kitalu (greenhouse) unafanyika muda wote

·       Kutafuta masoko ya bidhaa za shamba na kuhakikisha mazao yanafika sokoni kwa wakati

·       Kufanya kazi zingine utakazopangiwa na Mkuu wako wa kazi.

 

SIFA ZA MWOMBAJI:

·       Shahada/Stashahada ya kwanza ya kilimo au shahada ya Sayansi aliyejiimarisha katika mchepuo wa kilimo au fani inayoendana na hiyo kutoka kwenye chuo kinachotambulika na serikali

·       Uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika kazi.

·       Uzoefu wa vitendo katika shamba na ustadi katika uendeshaji na kutunza vifaa/mitambo ya kilimo

·       Cheti cha mafunzo katika Kilimo, Uendeshaji wa Mashine, Dawa n.k

·       Ujuzi katika matumizi ya kompyuta

·       Uzoefu katika Nyanja ya kilimo, uzalishaji wa mazao

·       Mkristo mwenye moyo wa kutumika Kanisani

·       Ujuzi wa kutumia kompyuta (word, Excel)

·       Umri usiozidi miaka 45

·       Ufanisi katika kazi na uwezo wa kufanya kazi Zaidi ya moja.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:

Waombaji wenye sifa watume Barua za Maombi ya kazi, Vivuli vya Vyeti na Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wao wa Dini kwa:

KATIBU MKUU,

KKKT – DAYOSISI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA

S.L.P 423

MWANZA.

                        KUPITIA BARUA PEPE: elctelvd84@gmail.com  

NB: Maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine tofauti na barua pepe HAYATAPOKELEWA!

TAREHE YA TANGAZO: 16/03/2025

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: Ijumaa Tarehe 04/04/2025         SAA: 04:00 Asubuhi

                                                                                                                     

ü  KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.

Mission Statement

ELVD endeavours to spread the gospel of Jesus Christ, through word and deed, to serve all people in the regions of Mwanza, Geita regions.

UPCOMING EVENTS

Feb 14

Marriage revival 2025

Friday 07:00 AM

Details →

Jan 19

Utambulisho wa Askofu na Msaidizi wa Askofu kwa Prof. Kabudi

Sunday 01:46 PM

Details →