NAFASI YA KAZI
KKKT- Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P 423 Mwanza
Tel/Fax + 255 28 2540674
Barua pepe: info@elvd.net
Tovuti: www.elct-elvd.org
Taarifa kuhusu DMZV: Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria ni moja kati ya Dayosisi 27 za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. DMZV inajumuisha mikoa miwili ya Mwanza na Geita.
DIRA YA DMZV: ‘Kuungana katika Kristo ili ufalme wa Mungu utawale.
DHIMA YA DMZV: Kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa maneno na matendo kwa watu wote katika mikoa ya Mwanza na Geita na kwingineko.
Mwanza Lutheran Secondary School: Ni shule inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria. Shule inatoa Elimu ya Sekondari kidato cha I – IV. Inapatikana eneo la Mabatini, Wilaya ya Ilemela-Mwanza.
Charming Safari (T) Ltd: Kampuni ya uwekezaji yenye usajili na kuendeshwa kwa taratibu na sheria za kampuni za nchi inayomilikiwa na Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania – Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria. Kampuni inatoa huduma ya safari za kitalii, hoteli na huduma ya uwakala wa fedha.
Uongozi wa Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria unatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:
v NAFASI YA KAZI: Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kilutheri Mwanza (MLSS)
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: Shule ya Sekondari ya Kilutheri Mabatini- Mwanza
ATARIPOTI KWA: Mkuu wa Idara ya Huduma za Jamii
ATAWAJIBIKA KWA: Bodi ya Shule & Meneja wa Shule
WAJIBU WA KAZI:
· Kusimamia utekelezaji wa mtaala
- Kuwa Mkaguzi wa ndani na wa awali wa program za ufundishaji wa walimu.
- Kupokea na kusajili wanafunzi wapya.
- Kusimamia mali zote za shule.
- Kutafsiri, kusimamia na kutekeleza Sera, sheria, ya Elimu, Kanuni na nyaraka mbalimbali za elimu.
- Kuandaa, kusambaza na kutumia taarifa na takwimu za shule kwa wakati na zikiwa sahihi.
- Kukusanya na kusimamia mapato na matumizi ya fedha za shule kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu
- Kuandaa, kusimamia na kuendesha mafunzo ya ndani kwa walimu ikiwa ni pamoja na kutoa “orientation” kwa walimu wapya.
- Kusimamia ustawi wa walimu na wanafunzi ili kila mmoja awajibike na apate haki zake zote kadri inavyowezekana.
- Kuandaa mpango kazi wa shule na taarifa za kila miezi mitatu na mwaka na kuwasilisha kwa Mkuu wa Idara Huduma za Jamii
- Kuwa kiungo kati ya shule, jamii na serikali
- Kuwa Katibu wa vikao vya Bodi ya Shule na kutekeleza mapatano ya vikao
- Kufundisha masomo aliyosomea ili kuwa mfano (model) na kuimarisha ualimu wa Mkuu wa Shule.
- Kusimamia na kudumisha nidhamu kwa wanafunzi na maadili kwa walimu ili kurejesha heshima ya ualimu.
- Kuboresha mazingira ya shule na kubuni njia za kuimarisha uendeshaji wa shule
- Kusimamia ukarabati wa miundombinu ya shule yakiwemo majengo na madawati ili yawe katika hali bora wakati wote
- Kufanya tathimini ya wazi (Open Performance review and Appraisal System OPRAS) utendaji kazi ya walimu na wafanyakazi wengine katika shule walio chini ya usimamizi wako
- Kupanga kazi za kitaaluma za mwaka kwa kushauriana na wafanyakazi, kuandaa na kusimamia vikao vya pamoja vya wafanyakazi katika shule
· Kufanya kazi zingine zinazopangwa na msimamizi
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Shahada ya kwanza katika fani ya Elimu kutoka katika chuo kinachotambulika na serikali.
· Uzoefu wa kazi angalau miaka miwili 2 na kuendelea
· Umri kuanzia miaka 30-50
· Ujuzi wa kutumia kompyuta
· Ufanisi katika kazi na uwezo
· Uwezo mzuri katika mawasiliano
· Elimu/Ufahamu katika sheria na miongozo ya Elimu ya nchi
v NAFASI YA KAZI: Meneja wa Kampuni (Utalii & Hoteli)
IDADI YA NAFASI ZA KAZI: Moja (1)
MAHALI PA KAZI: Charming Bungalow Hotel- Nyakato-Mwanza
ATARIPOTI KWA: Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji
ATAWAJIBIKA KWA: Bodi ya Kampuni
WAJIBU WA KAZI:
· Kupanga na kusimamia kazi za kila siku za Kampuni
· usimamia na kutekeleza mapatano ya vikao vya Bodi ya Kampuni kwa kuzingatia Mpango kazi na Mpango Mkakati
· Kusimamia na kuhakikisha usalama wa eneo la kazi
· Kusimamia na kufanya tathimini za kazi za wafanyakazi wa Kampuni
· Kubuni njia mbalimbali za uendeshaji wa miradi inayosimamiwa na Kampuni
· Kusimamia na kudumisha uhusiano mzuri wa wageni na wateja
· Kusimamia na kufuatilia orodha na mali za Kampuni
· Kuandaa, kusimamia na kutengeneza bajeti za uendeshaji wa Kampuni kwa kushirikiana na wafanyakazi
· Kufanya tathimini za kawaida za uboreshaji wa Huduma ya wateja
· Kukusanya malipo na kudumisha kumbukumbu za bajeti, fedha na gharama
· Kuandaa ripoti na taarifa ya kazi ya Kampuni ya miezi Mitatu, Sita, Tisa na Mwaka kwa kushirikiana na wafanyakazi wa miradi husika
· Kuandaa Mpango kazi wa mwaka na Mpakgo Mkakati wa Kampuni na kusimamia utekelezaji wake
· Kushughulikia malamiko na maswali ya wateja ili kukuza biashara
· Kusimamia na kufuatiliaji taratibu na matakwa ya kisheria ya uendeshaji wa Kampuni
· Kuandaa taarifa ya mapato na matumizi ya kila mwezi ya Kampuni kwa kushirikiana na Mhasibu wa Kampuni
· Kutoa ushirikiano katika zoezi la ukaguzi wa hesabu na nyaraka muhimu za Kampuni kwa mkaguzi wa ndani na nje
· Kufanya kazi zingine utakazo pangiwa na Msimamizi/Mwajiri
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Shahada/Stashahada ya Usimamizi wa Biashara, Rasilimali watu, Masoko, Usimamizi wa Hoteli, Utalii au fani nyingine zinazoendana kutoka katika chuo kinachotambulika na serikali
· Wenye Cheti cha usimamizi wa Hoteli/Hotel Management) au Utalii(Tourism) watapewa kipaumbele
· Uwezo mzuri wa mawasiliano ya kutunza mitandao kama barua pepe, facebook, instagram, twitter na kufanya booking.
· Uwezo mzuri wa kuhudumia na kuzungumza na wateja kwa ukarimu/Good Customer Care and Hospitality)
· Uzoefu wa kazi angalau miaka mmoja na kuendelea katika usimamizi wa Hoteli, usimamizi wa Rasilimali watu, Utalii/Biashara
· Uelewa mzuri wa sheria ya Kampuni/Company Law
v NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:
Waombaji wenye Sifa Watume/Kuwasilisha Maombi ya kazi kwa:
KATIBU MKUU KKKT-DMZV
S.L.P 423, MWANZA
Kupitia Barua Pepe: elctelvd84@gmail.com
NB: Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya Barua Pepe:
Muombaji wa Nafasi ya kazi atatakiwa kuwasilisha vitu vifuatavyo:
· Barua ya Maombi ya Kazi,
· Wasifu/CV
· Vivuli vya Vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria (Certified Certificates)
· Barua ya Utambulisho kutoka kwa kiongozi wa Dini/Mahali anapo abudu
TAREHE YA TANGAZO: 04/06/2025 MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 24/06/2025
ü KKKT- DMZV inatoa fursa za ajira kwa watu wote wenye sifa.