TANGAZO LA ZABUNI YA KUSAMBAZA CHAKULA WAKATI WA MKUTANO MKUU WA DMZV UTAKAOFANYIKA TAREHE 26/07/2024
Uongozi wa KKKT-DMZV unapenda kuwatangazia na kuwakaribisha wazabuni wenye nia na uwezo wa kusambaza chakula wakati wa maandalizi na siku ya Mkutano Mkuu wa DMZV utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 26/07/2024 eneo la Mkutano ni Usharika wa Ebenezer - Pansiansi Jimbo la Mwanza Kati. Tunakaribisha wazabuni wanaotimiza vigezo na masharti katika tangazo hili kuwasilisha nyaraka zao.
SIKU |
TAREHE |
AINA YA CHAKULA |
IDADI YA WATU |
ALHAMISI |
25/07/2024 |
CHAKULA CHA USIKU (DINNER) |
100 |
IJUMAA |
26/07/2024 |
CHAI NA CHAKULA CHA MCHANA |
250 |
CHAKULA CHA USIKU (DINNER) |
200 |
||
JUMAMOSI |
27/07/2024 |
CHAI YA ASUBUHI (BREAKFAST) |
100 |
1. Zabuni hii itashindanishwa kitaifa (National Competitive)
2. Zabuni hii ya kusambaza chakula itaanza kupokelewa rasmi tarehe 01/06/2024 Saa 02:00 Asubuhi
3. Tarehe ya mwisho ya kupokea zabuni itakuwa Alhamisi tarehe 13.06.2024.
4. Zabuni zitafunguliwa siku ya Ijumaa tarehe 14.06.2024 saa 4.30 Asubuhi.
5. Zabuni zifungwe vizuri (sealed) kwenye bahasha na juu ya bahasha iandikwe zabuni ya kusambaza chakula wakati wa Mkutano Mkuu wa KKKT - DMZV na zitumbukizwe katika sanduku la zabuni litakalokuwa katika veranda nje ya ofisi ya Katibu Mkuu wa KKKT – DMZV katika jengo la UTAWALA.
6. Ndani ya Bahasha ya zabuni viambatanishwe vifuatavyo vikiwa vyote vinasoma jina la mzabuni;
ü Nakala ya namba ya utambulisho wa Mlipa kodi
ü Nakala ya leseni ya Biashara
ü Nakala ya Profoma Invoice
ü Nakala tupu ya Invoice
ü Nakala tupu ya Delivery note
ü Kithibitisho cha kumiliki risiti ya mashine (EFD receeipt)
7. Ada ya zabuni ni shs. 20,000/- iwekwe kwenye a/c ELCT-ELVD General Administration No. 0150355080301 CRDB Bank – na ‘pay in slip’ ya benki iambatanishwe na barua ya maombi ya zabuni.
8. Kwa mawasiliano zaidi piga simu +255 623 850 509
Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu
KKKT – Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria
S.L.P. 423, Mwanza.